Rais wa klabu ya Salernitana Danilo Iervolino amesema kuwa mchezaji wa klabu hiyo Franck Ribery atasalia Salernitana ambapo atachukua nafasi ambayo itakuwa sio ya kuichezea klabu hiyo.

Ripoti zimesema winga huyo wa Kifaransa mwenye umri wa miaka 39, ambaye ni nahodha wa kikosi cha Serie A, anaweza kutangaza kustaafu mapema wiki ijayo baada ya kusumbuliwa na majeraha ya goti.
Baada ya kujiunga na Salernitana kutoka Fiorentina mwaka jana, mchezaji huyo wa zamani wa Kimataifa wa Ufaransa amecheza mara mbili pekee katika mashindano yote msimu huu, na kushindwa kutokea tangu Agosti.

Sasa inaonekana kwamba muda wake uwanjani unakaribia kumalizika lakini Iervolino amefichua majadiliano yamefanyika kuhusu uwezekano wa yeye kuchukua nafasi ya nyuma. “Tunazungumza sisi kwa sisi,” aliiambia DAZN. “Frank ni bingwa mzuri ndani na nje ya uwanja, na anafanikiwa kuleta bora zaidi kwa kila mtu.
Kocha mkuu wa Salernitana aliongeza kwa kusema Ribery ni kiongozi hivyo watamuweka katika nafasi anayotaka. Mchezaji huyo ana hadhi ya juu sana kwamba ataweza kukaa nafasi yoyote.

Mshindi mara tisa wa Bundesliga akiwa na Bayern Munich, Ribery amecheza mechi 25 katika mashindano yote akiwa na Salernitana tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2021.

