Yanga Yazidi Kujikita Kileleni Baada ya Kuichapa Geita Gold

Klabu ya Yanga ambayo ipo chini ya kocha mkuu Nasredine Nabi imezidi kujiweka kileleni kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuichapa Geita Gold mabao 3-1 hapo jana.

 

Yanga Yazidi Kujikita Kileleni Baada ya Kuichapa Geita Gold

Mchezo huo uliochapwa katika uwanja wa Chamazi Complex ulikuwa wa kuvutia kwa pande zote mbili huku wananchi wakitokea nyuma baada ya kuchapwa bao katika dakika za kipindi cha kwanza cha mchezo na Maguli.

Wakati kwa upande wa Yanga mabao hayo ya kuichabaga Geita Gold yalitupiwa kimyani na Kennedy Musonda, Mzize pamoja na Moloko na kuwafanya wafikishe pointi 65 kwenye msimamo wakiwa mbele kwa pointi 8 kwa anayemfuata.

Yanga Yazidi Kujikita Kileleni Baada ya Kuichapa Geita Gold

Baada ya ushindi wa jana sasa Young Africans wameshinda michezo 11 mfululizo kwenye ligi na kuweka historia hiyo ambapo mchezo wa mwisho kufungwa ilikuwa ni dhidi ya Ihefu Novemba 29.

 

Acha ujumbe