Alan Shearer: Rashford Anakosa Ukatili Mbele ya Lango

Gwiji wa zamani wa soka la Uingereza na klabu ya Newcastle United Alan Shearer amesema haamini kama mshambuliaji wa kalbu ya Manchester United Marcus Rashford ana uhatari wa kuongoza safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.

Marcus Rashford ambaye ameshafunga magoli mawili tangu arejee kwenye michuano ya kombe la dunia, Mshambuliaji huyo amefanikiwa kufunga bao katika mchezo wa Carabao siku ya Jumatano dhidi ya Burnley na jana akifanikiwa kufunga bao dhidi ya Nottingham Forest kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza.alan shearerMarcus Rashford ambaye anaonekana ni kama amezaliwa upya kwani mpaka sasa ameshafunga mabao 10 msimu huu ambapo msimu uliomalizika alifunga mabao matano msimu mzima, Huku pia akiwa amepiga pasi nne za mabao hivo tayari kahusika kwenye mabao 14 mpaka sasa msimu huu.

Licha ya ubora ambao ameonesha Rashford msimu huu ila bado haujamshawishi gwiji Alan Shearer kuamini kama mchezaji huyo anaweza kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Manchester United kwasababu anakosa ukatili mbele ya lango.alan shearerMfungaji bora wa muda wote kwenye ligi kuu ya Uingereza Alan Shearer anasema kwasasa mshambuliaji huyo ana uhuru wa kucheza na anaonekana kufurahia kutokea kushoto, Lakini amemtaka kocha wa timu hiyo Erik Ten Hag kutafuta mshambuliaji mwenye ubora zaidi kwenye eneo la katikati kwakua anaamini Rashford bado hawezi kubeba majukumu hayo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.