Klabu ya Arsenal imefanikiwa kumtambulisha aliyekua beki wa klabu ya Ajax Jurien Timber ambaye amesajiliwa klabuni hapo kwa dau la euro milioni 45.
Timber amejiunga na Arsenal rasmi leo na kutambulishwa lakini ni mchakato uliochukua wiki kadhaa mpaka kukamilika, Beki huyo amechagua kujiunga na Washika mitutu hao kutoka jiji la Londo licha ya kufuatiliwa na vilabu kadhaa.
Jurien Timber amefurahi kujiunga na klabu hiyo kutoka Kaskazini mwa London na kwa mchezaji huyo ilikua hana kipaumbele kingine zaidi ya klabu hiyo kama angeondoka ndani ya klabu ya Ajax majira haya ya joto.
Arsenal katika majira haya ya joto mwaka huu wameonekana kua makini sana na kutumia pesa kwa kiwango kikubwa, Kwani Timber anakua mchezaji wa tatu kusajili klabuni hapo baada ya Kai Havertz na Declan Rice.
Jurien Timber amekua kwenye kiwango kizuri sana na klabu yake ya zamani ya Ajax kwa misimu kadhaa, Hivo Arsenal wao wakaona ni mtu sahihi wa kuja kuongeza nguvu kwenye safu yao ya ulinzi kuelekea msimu ujao.

