Mendy Akutwa hana Hatia

Beki wa klabu ya Manchester City na timu ya taifa ya Ufaransa Benjamin Mendy amekutwa hana hatia baada ya kushutumiwa kuhusika na unyanyasaji wa kingono.

Mendy alishtumiwa kuhusika kwenye suala la unyanyasaji wa kingono kwa takribani miaka miwili nyuma, Lakini mapema leo mahakama imeamuru mchezaji huyo hana hatia kutokana na kesi ambazo zilikua zinamkabili ambazi zilikua zaidi ya moja.MendyMchezaji huyo amekutwa hana hatia baada ya kukabiliwa na kesi hizo hivo ni wazi ataweza kurejea kuanza kucheza mpira wa miguu baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takribani miaka miwili sasa taarifa kutoka klabu yake ya Manchester City itakuja kutoa ufanunuzi zaidi juu ya mustakabali wa mchezaji huyo.

Benjamin Mendy alikua mchezaji mwenye uwezo mkubwa kabla ya kukumbana na kashfa hiyo ya unyanyasaji wa kingono, Hivo inawezekana akaendelea kuitumikia klabu yake ya Manchester City msimu ujao au akaondoka na kucheza timu nyingine.MendyWachezaji mbalimbali wameonekana kuhuzunishwa na kitendo kilichomkuta Mendy kwa mfano Memphis Depay ambaye amehoji kua baada ya beki huyo kupoteza miaka miwili nje ya uwanja na kukutwa hana hatia nani atalipia matatizo yote yaliyomkuta na kutaka kuwepo kwa watu watakaoshughulikia jambo hilo mapema kabla ya madhara kutokea.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.