Golikipa na nahodha wa klabu ya Tottenham Hugo Lloris ataondoka ndani ya klabu ya hiyo mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu.
Golikipa Lloris ameomba ruhusa ya kutosafiri na timu kuelekea maandalizi ya msimu ujao kwajili a kupambana kwajili ya kutafuta timu ya kuelekea msimu ujao ambapo hatakua kwenye klabu hiyo kutoka kusini mwa jiji la London.
Kipa huyo ameitumikia klabu ya Tottenham kwa muda mrefu sasa na anahitaji kupata changamoto mpya katika timu nyingine msimu ujao, Ikiwa ndio sababu ya kuomba kuondoka ndaani ya viunga vya Tottenham kuelekea msimu ujao.
Golikipa Hugo Lloris amecheza kwa kiwango kikubwa ndani ya Tottenham kwa miaka mingi lakini hakuwahi kushinda taji la aina yeyote zaidi ya kucheza fainali ya ligi ya mabingwa ulaya mwaka 2019 pamoja na kombe la Carabao.
Ofa mbalimbali kutoka nchini Saudia Arabia zinaelezwa kufika mezani kwa golikipa huyo mshindi wa kombe la dunia akiwa kama nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Lakini golikipa huyto hajafanya maamuzi ya wapi atakwenda msimu ujao.

