Arsenal Yajitoa Mhanga kwa Caicedo

Klabu ya Arsenal imejitoa mhanga kuwania saini ya kiungo wa kimatifa wa Ecuador anayekipa katika klabu ya Brighton and Hove Albion Moises Caicedo katika dirisha la mwezi Januari.

Klabu ya Arsenal ipo kwenye mpango wa kumsajili kiungo wa klabu ya Brighton Moises Caicedo na wameweka dau la Euro milioni 60 ili kumnasa kiungo huyo ambaye anaonesha ubora mkubwa ndani ya ligi kuu ya Uingereza. Hivo washika mitutu wa London wanataka kuboresha kikosi cha ndani ya dirisha hili la mwezi Januari.caicedoKiungo Moises Caicedo ni miongoni mwa viungo wanaofanya vizuri sana kwenye klabu ya Brighton and Hove Albion pamoja na ligi kuu ya Uingereza kwa ujumla, Hivo klabu ya Arsenal wanamuhitajji kiungo huyo zaidi kwasababu ya ubora ambao anauonesha.

Kuumia kwa Mohamed Elney inaweza kua sababu kubwa ya washika mitutu wa London kuhitaji saini ya Moises Caicedo, Kwani kama ataumia kiungo anayeanza ndani ya klabu hiyo Thomas Partey basi itakua vigumu kwa klabu hiyo kufanya vizuri kutokana kutokua na benchi imara na lenye wachezaji wenye ubora.caicedoMoises Caicedo alieleza siku kadhaa nyuma kua ana mipango ya kuendelea kubaki ndani ya klabu yake ya Brighton Hove and Albion kutokana na namna anavyopata nafasi ya kucheza kila wiki, Lakini Arsenal ni kama wameweka pamba masikioni na kutuma ofa ya kumuhitaji kiungo ili akawatumikie ndani ya klabu yao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.