Arteta: Tunatakiwa kua na Ufanisi

Kocha wa klabu ya Arsenal Mikel Arteta anasema wanapswa kua wafanisi zaidi baada ya kupoteza mchezo wao wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Manchester City siku ya Jumatano.

Klabu ya Arsenal iliondolewa kileleni na klabu ya Manchester City iliwashusha Arsenal kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kuwafunga mabao matatu kwa moja, Lakini kocha Arteta anataka kuchukua mazuri katika mchezo huo waliopoteza na sio mabaya ili yaweze kuwasaidia katika michezo yao inayofuata.ArtetaKlabu ya Arsenal ya Arsenal sasa imetimiza michezo minne bila kupata matokeo ya ushindi kwenye michuano yote, Huku wakipoteza michezo mitatu na kusuluhu mchezo mmoja kitu kinachowafanya kua na wakati mgumu kuelekea michezo inayofuata.

“Ninajua mambo sahihi ya tunayopaswa kufanya ili kuendelea kua pale juu, Nimeona kiwango kiko wapi na tunapaswa kufanya nini ili kurejea kwenye kiwango hicho, Kuna mazuri mengi ya kuchukua kuanzia mwanzo wa msimu na mpaka kupoteza dhidi ya City. Tunajua kiwango cha ufanisi kinapaswa kua juu kila mchezo ili kuwashinda City mwishoni” Maneno yya kocha Mikel Arteta akeileza kua wanapaswa kufanya viuri katika michezo yao inayofata ili kuwashinda Man City.ArtetaKlabu ya Arsenal itakua ugenini kumenyana na klabu ya Aston Villa ambayo inafundishwa na mkufunzi wa zamani wa klabu hiyo Unai Emery, Hivo wanapaswa kua macho ili kuhakikisha wanarudi kwenye njia yao ya ushindi ambayo kocha Arteta anaamini wanaweza kurejesha fomu yao waliyokua nayo siku zilizopita.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.