Klabu ya Atletico Madrid ambayo ipo chini ya kocha wake mkuu Diego Simeone, yashindwa kufuzu hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kutoa sare ya 2-2 hapo jana dhidi ya Bayer Leverkusen .

 

Atletico Madrid Yashindwa Kufuzu Hatua ya 16 Bora Baada ya Sare ya Jana.

Atletico walitanguliwa kufangwa bao katika dakika ya 9 ya mchezo , na wakaja kusawazisha katika dakika ya 22 lakini baada ya kuzembea tuu walijikuta wanaenda mapumziko wakiwa nyuma ya bao moja baada ya Odoi kuifungia timu yake bao la pili.

Dakika ya 50 ya mchezo wanapata bao la kusawazisha kupitia kwa De Poul na kufanya ubao usomeke 2-2 ambapo hadi dakika 90 za mchezo ikawa ni mbili kwa mbili. Katika dakika ya 90+9 wanapata zawadi ya penati ambayo ingewafanya wakawa na matumaini lakini Carrasco anakosa mkwaju ule wa penati na kuwafanya washindwe kusonga mbele.

Atletico Madrid Yashindwa Kufuzu Hatua ya 16 Bora Baada ya Sare ya Jana.

Kwahiyo sasa, Atletico katika kundi lao B waliofuzu ni Club Brugge mwenye pointi 10 akifuatiwa na FC Porto mwenye pointi 9, huku yeye na Leverkusena wakiwa na kibarua cha kugombania nani atacheza Europa.

Ili sasa Simeone na vijana wake wacheze michuano ya Europa inabidi mechi ya mwisho washinde ambayo itakuwa ni dhidi ya FC Porto, Wakati kwa upande wa Leverkusen yeye atahitajika kucheze dhidi ya Club Brugge. Bado mambo ni magumu kwa upande wa nani kwenda Europa.

Atletico Madrid Yashindwa Kufuzu Hatua ya 16 Bora Baada ya Sare ya Jana.

Mechi inayofuata kwenye Laliga Atletico watakabiliana na Cadiz wakiwa ugenini, wakati kwa Leverkusen wao watacheza dhidi ya RB Leipzig kwenye Bundesliga.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa