Ligi kuu ya NBC kuendelea hii leo kwa mchezo mwingine mmoja hii leo ambapo ni Dabi ya Mzizima inayowakutanisha Azam Fc dhidi ya Simba katika mchezo wao Ligi kuu huku kwa upande wa Wekundu wa Msimbazi ni mchezo wake wa 7 na kwa upande wa mwenyeji ni mchezo wake wa 8.

 

Azam FC Dhidi ya Simba ni Leo Oktoba 27.

Azam FC ambaye ametoka kumtimua kocha wake baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya KMC kwa mabao mawili kwa moja na kuwa na matokeo ambayo hayarodhishi kama klabu, anahitaji mchezo huu kwa hali na mali ili aweze kujiweka kwenye nafasi nzuri.

Wakati kwa upande wa Simba nae anahitaji mchezo huu ili aweze kukaa kileleni baada ya kutoa sare ya moja kwa moja dhidi ya mahasimu wao wakuu Yanga, ambao wameshinda jana na kuongoza Ligi.

Azam FC Dhidi ya Simba ni Leo Oktoba 27.

Mchezo huo utapigwa majira ya saa 1:00 usiku kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Azam waliamua kuuhamishia hapo kwaajili ya watu wengi waweze kuhudhuria mechi hiyo pia na sheria kuruhusu.

Simba hajapoteza mchezo wowote mpaka sasa kwenye Ligi, ambapo wameshinda michezo  minne, sare mbili baada ya michezo sita na wana pointi 14. Na hata pia baada ya ujio wa Juma Mgunda hajapoteza pia. Kwa upande wa Wanalambalamba wao wamepoteza michezo miwili sare mbili na ushindi mara tatu, pointi 11 huku wakiwa nafasi ya 9 kwenye msimamo.

Azam FC Dhidi ya Simba ni Leo Oktoba 27.

Kwahiyo leo hii, Azam wataingia uwanjani wakiwa chini ya usimamizi wa muda wa Kali Ongala pamoja na Agrey Moris kabla ya kumpata kocha mpya ambae atarithi nafasi ya aliyekuwa kocha wao Denis Lavagne.

Mechi 5 za mwisho kukutana timu hizi mbili, Azam hajashinda hata mechi moja, Simba ameshinda mechi mbili na Wametoa sare tatu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa