Mchezo wa ligi kuu Bara kati ya Azam dhidi ya Simba unaotarajiwa kupigwa Oktoba 27 mwaka huu sasa utapigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Azam ambao ni wenyeji wa mchezo huo wamehamisha mchezo huo ambao awali ulikuwa upigwe kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi.
Akizungumzia Mabadiliko ya mchezo huo, Ofisa Habari wa Azam, Hasheem Ibwe amesema mchezo huo sasa utapigwa kwenye Uwanja wa Mkapa.
“Kuna mabadiliko yamefanywa na uongozi ambapo mechi ya ligi inayofuata dhidi ya Simba itapigwa kwenye uwanja wa Mkapa badala ya Chamazi.
“Sababu ya mabadiliko hayo ni maslahi ya timu pia kuwapa fursa mashabiki wetu kuweza kuja uwanjani kwa wingi ili kuisapoti timu yao.”