Klabu ya Azam FC imetangaza kuwa mchezo wao dhidi ya Simba ambao ulitarajiwa kupigwa katika uwanja wa Chamazi Complex, tarehe 27 Oktoba, sasa utapigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa siku ya Alhamisi majira ya saa 1:00 usiku.

 

Azam Yapeleka Mechi Yao Dhidi ya Simba kwa Mkapa.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Afisa Habari wa Azam, Hasheem Ibwe ameandika na kusema kuwa sababu kuu ya kupeleka mechi hiyo katika uwanja wa Mkapa ni maamuzi ya klabu binafsi ambayo pia kikanuni ianaruhusiwa kuchagua uwanja wa nyumbani kucheza mechi yao.

Pia aliongezea kwa kusema sababu nyingine ni kutoa wigo mpana zaidi kwa mashabiki wao na wa Simba kuja kuona mpira ukipigwa katika siku hiyo.

Ikumbukwe kuwa Azam FC wametoka kupoteza mechi yao dhidi ya KMC ugenini ambapo kutokana na matokeo hayo yamefanya wamfukuze aliyekuwa kocha wao Lavagne ambaye hata hakufikisha miezi miwili tangu ajiunge na timu hiyo.

Azam Yapeleka Mechi Yao Dhidi ya Simba kwa Mkapa.

Kwahiyo timu hiyo ipo chini ya Sam Daniel Ongala na Agrey Moris mpaka pale watakapotangaza vinginevyo. Wanalambalamba hao ambao makazi yao yapo Chamazi mpaka sasa wapo nafasi ya 5 baada ya kucheza mechi 7, wameshinda 3, sare 2 na wamepoteza michezo 2 na wamejikusanyia pointi 11.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa