UONGOZI wa klabu ya Azam umeachana na Kocha Mkuu, Denis Lavagne raia wa Ufaransa kutokana na matokeo mabaya yaliyoiandama klabu hiyo hivi karibuni.

Lavagne alianza kukinoa kikosi hicho Septemba 6 mwaka huu akichukua mikoba ya aliyekuwa Kocha Mkuu, Abdihamid Moallin baada ya kutimuliwa.

Azam, Azam Yamtimua Mfaransa, Meridianbet

Katika michezo sita aliyosimamia kocha huyo tangu atue nchini amefanikiwa kushinda mitatu na kupoteza michezo mitatu.

Azam FC kwa sasa inanolewa na Kaimu Kocha Mkuu, Kali Ongala akisaidiwa na Agrey Moris katika kipindi hiki ambacho timu huyo haina Kocha Mkuu.

Kikosi cha Azam ambacho tayari kimeanza mazoezi jana jumapili kinatarajia kucheza mchezo ujao wa ligi dhidi ya Simba.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa