Beki wa kulia wa kulia wa klabu ya Simba, Shomari Kapombe amerejea mazoezini kwa kasi baada ya kupata majeraha ambayo yamemuweka nje ya uwanja kwa muda kidogo na kukosa baadhi ya mechi ikiwemo ya Dabi ya Kariakoo.
Shomari Kapombe ambaye ndiye mbavu muhimu ya kulia kwa upande wa Simba na tegemezi baada ya kuwa na kiwango bora kwa muda mrefu na kuwaaminisha mashabiki wa Wekundu wa msimbazi yeye ni bora ameanza mazoezi na wenzake.
Beki ambaye pia anaichezea timu ya Tanzania (Taifa Stars) mashabiki na wapenzi wa Simba wanatarajia kumuona pia akirejea uwanjani kutokana na nafasi yake aliyokuwa anacheza kuchukuliwa na Israel Mwenda ambaye nae pia alipata majeraha mechi iliyopita.
Taarifa zinasema kuwa Kapombe ataangaliwa kama anaweza kuanza leo au aingie akitokea benchi baada ya kuwa na wasiwasi wa Mwenda kuumia. Mgunda anatarajia kwenda kupata alama 3 muhimu huku toka ajiunge na timu hiyo hajapoteza mchezo wowote.
Tofauti kati yao ni pointi 3 ambapo Simba ana pointi 14, wakati wa Azam ana pointi 11 huku akiwa amezidi mchezo mmoja.