Shomari Kapombe Alivyonikumbusha Nukuu ya Albert Einstein

Ya kwanza BISMILLAH, ni kwa Jina la Mwenyezi Mungu mwenye kubariki vitu vyote na kumpa yule amtakae, ni yeye atasema liwalo liwe au lisiwe, ni yeye ataamuwa hata ukipora jua itapotea ili mradi yatimie maandiko

Mwenyezi Mungu aliumba Wanadamu kisha akamuumba Mwanasayansi Albert Einstein, binadamu huyu alisema “everybody is a genius. But if you judge a fish by its ability to climb a tree, it will live its whole life believing that it is stupid”

Basi waambieni Watu waweke kalamu zao vyema, waandae karatasi vyema wanapotaka kumjadili Shomari Salum Kapombe, kuna namna dunia imechoka inalazimisha atokee mtu awe zaidi ya Kapombe lakini bado sana kwasasa na sioni ikitokea karibuni

Naendelea kufurahia kazi ya macho yangu kama Shomari anaweza kucheza beki ya kulia na akateleza kama Anaconda na misitu ya Amazon, naendelea kutabasamu nikimuona kwenye eneo la Kiungo akipokea pass kama Mafikizolo na kuzipiga kama kinanda cha Mozart

Enyi Mashabiki kuna dhambi zinaepukika ukiachana na dhambi kuu ya kudhini, basi hii dhambi ya kuamini kuna mbavu ya kulia kama Shomari tujiepushe nayo, tuendelee kufurahia kwakuwa watu kama hawa huzaliwa mara chache, kwenye nchi chache na kwa nyakati chache

Wapo vijana wanakuja ila bado Shomari ni Marking scheme yao, unataka kuwa bora mtazame Shomari, unataka kucheza kwa muda mrefu basi mtazame Shomari, umewahi kupitia majaribu ya soka na hujui utashinda vipi? Basi mpigie simu Shomari, atakwambia kila kitu

Acha niendelee kufurahia kazi ya macho yangu, kama ambavyo Madaktari wa Afrika Kusini walivyopitisha kisu kwenye mwili wa Shomari kumaanisha kuwa mpira bado unamdai, kama ambavyo alijiondoa Stars na kurudi tena kumaanisha kuwa nchi bado inamdai vingi.

Kila Binadamu ana ubora wake ila tukimlaumu Samaki kwanini hapandi mtini, basi Samaki ataishi maisha yake yote kujua kuwa hana akili, kifupi alimaanisha kila Mtu ana ubora na upungufu wake na sio lazma afanane na mwingine, alimaanisha hivyo Albert Einstein


MSHINDANI HUSHINDA BWANA!

Anayejaribu hawezi kutoka kapa Meridianbet! Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet inakuhakikishia ushindi mkubwa kila unapojaribu kuingia mchezoni. Washindi hushindana, ingia mchezoni!

Fairy-in-Wonderland_Casino-Post_25-January

CHEZA SASA

13 Komentara

    Wapo vijana wanakuja ila bado Shomari ni Marking scheme yao, unataka kuwa bora mtazame Shomari, unataka kucheza kwa muda mrefu basi mtazame Shomari, umewahi kupitia majaribu ya soka na hujui utashinda vipi? Basi mpigie simu Shomari, atakwambia kila kitu

    Jibu

    Kapombe ni mtu hatari

    Jibu

    Shomari Yuko makini na kazi yake

    Jibu

    Shomari kijana yuko vzr

    Jibu

    Kapombe yupo vizuri

    Jibu

    Salute kwa Mwandishi

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Imeeleweka

    Jibu

    Abari nzuri

    Jibu

    Kapombe yuko poa

    Jibu

    Kapombe Yuko vizuri

    Jibu

    HAbar nzur snaa

    Jibu

    Shomar kama shomar

    Jibu

Acha ujumbe