Klabu ya Tottenham Spurs walilazimika kusubiri VAR iamue hatma yao ya kufuzu hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye mchezo dhidi yao na Sporting Lisbon ya Ureno baada ya goli la ushindi la Harry Kane dakika ya 95 kukataliwa na mwamuzi wa mchezo huo.

 

Spurs Yatoa Sare Huku VAR Ikimpatia Conte Kadi Nyekundu.

Vurugu zilianza baada ya goli kukataliwa kweny mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1, huku Spurs wakitokea nyuma ya bao moja ambalo walikuwa wameshapigwa dakika ya 22 ya mchezo na kusubiri hadi dakika ya 80 ndipo wakapata bao la kusawazisha.

Dakika ya 95 wanapata bao lakini VAR inakataa bao hilo na kusema kuwa mshambuliaji huyo alikuwa ameotea na kusababisha mshangao mkubwa kwa timu huku kocha mkuu wa klabu hiyo Antonio Conte akipewa adhabu ya kadi nyekundu.

Klabu ya Sporting walipoteza nafasi nyingi za kujihakikishia pointi ambazo zingewafanya wawe vinara wa kundi hilo.Kundi D ndio kundi ambalo linaonekana kuwa moja ya makundi magumu zaidi ya Ligi ya Mabingwa, kutokana na kuwa kila timu kwenye kundi hilo ana uwezo wa kwenda 16 bora huku kukiwa na mchezo mmoja umebaki kwa kila timu.

Spurs Yatoa Sare Huku VAR Ikimpatia Conte Kadi Nyekundu.

Spurs watacheza dhidi ya Marseille ambapo watakuwa ugenini huku tofauti yao ikiwa ni pointi mbili yoyote atakayeshinda atasonga mbele, huku akiwa ameshinda mechi mbili pekee kati ya nane zilizopita za Ligi ya Mabingwa, sare mbili na lupoteza mara mbili, kufuatia mfululizo wa ushindi mara tatu kati ya Oktoba na Novemba 2019.

Baada ya kupoteza kila mechi kati ya tano za kwanza za Ligi ya Mabingwa dhidi ya vilabu vya Uingereza, Sporting hawajafungwa katika mechi tatu kama hizo, wakiepuka kupoteza  dhidi ya Manchester City ambapo walipata sare moja kwa Spurs ushindi mara moja na sare moja.

Spurs Yatoa Sare Huku VAR Ikimpatia Conte Kadi Nyekundu.

Mechi inayofuata kwa Spurs baada ya sare ya jana ni dhidi ya Bournemouth kwenye Ligi kuu ya Uingereza siku ya Jumamosi ambapo watakuwa ni wageni wa mchezo huo, Wakati kwa upande wa Sporting wao watakupiga dhidi ya Arouca kwenye Ligi siku hiyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa