Mcheza Tenisi wa Belarus, Victoria Azarenka amesema kuwa marufuku ya Wimbledon kwa wachezaji kutoka Urusi na nchi yake haina mantiki na mchezaji huyo ametoa wito kwa bodi zinazosimamia tenisi kuchukua hatua dhidi ya uamuzi huo.

All England Lawn Tennis Club, ambao ni wenyeji wa Grand Slam ilichukua uamuzi huo kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na msimamo huo ulilaaniwa na men’s and women’s tours.

 

azarenka, Azarenka : Hakuna Sababu Kufungia Wachezaji Wimbledon., Meridianbet

ATP na WTA zilishutumu uamuzi huo kama wa kibaguzi, huku Steve Simon, mkuu wa women’s tour, wiki iliyopita akionya juu ya “athari kali”.

“Iwapo utaniuliza kama ninakubaliana na Wimbledon au ninaona hoja zao baada ya kuwapigia simu ya binafsi, sioni hoja zao,” alisema Azarenka, ambaye yuko kwenye baraza la wachezaji wa WTA, aliwaambia waandishi wa habari mjini Madrid.

“Haiingii akilini na haiunganishi kile wanachokisema.”

Azarenka 32, anayeshika nafasi ya 17 duniani, alishinda mechi yake ya ufunguzi kwenye hafla ya WTA 1000 huko Madrid siku ya Alhamisi, lakini Mbelarusi mwenzake Aryna Sabalenka alipoteza kwa seti 6-2 3-6 6-4 kwa Amanda Anisimova wa Amerika.


 

BURUDIKA NA KASINO BOMBA ZA MTANDAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa