Taarifa za hivi majuzi kutoka kwa maripota mbalimbali zilidai Paris Saint-Germain wapo mbioni kumuondoa kocha klabu hiyo Mauricio Pochettino lakini raia huyo wa Argentina amedai kwamba yeye na Kylian Mbappe wataendelea kuwepo PSG kwa asilimia 100.

Lakini aliongeza kwa kusema kwamba huu ni mpira wa miguu na huwezi kujua nini kitatokea.

Mbappe amekuwa akihusishwa kuikacha klabu hiyo na Real Madrid wamekuwa wakivutiwa kumnasa mshambuliaji huyo wa Ufaransa wakati wa dirisha la majira ya kiangazi na kandarasi yake inalekea kuacha kufanya kazi mwisho wa msimu huu.

Alipoulizwa ni kwa asilimia ngapi anaamini yeye na Kylian Mbappe wataendelea kusalia PSG msimu ujao Pochettino alisema: “Kwa asilimia mia kwa mambo yote.”

“Tunaendelea kufanya kazi kwa bidii, sio tu kwa kuzingatia sasa, lakini pia na jukumu la kufikiria juu ya siku zijazo, kwa hivyo ndivyo tunajua

FURAHIA KASINO MARIDHAWA ZA MERIDIANBET SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa