Tetesi zinasema, Arsenal inamtaka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford, 24.

Meneja wa Derby Wayne Rooney anasakwa na Burnley kama chaguo lao namba moja kumrithi Sean Dyche.

Manchester United imeipa ishara Napoli kwamba wako tayari kulipa £84m kwaajili mshambuliaji Mnigeria Victor Osimhen, 23.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema, Liverpool wanatarajia kumsajili kiungo mfaransa wa Monaco Aurelien Tchouameni, 22.

Kocha ajaye wa Manchester United Erik ten Hag anataka kumsajili mshambuliaji wa Juventus na Argentina Paulo Dybala, 28.

Tottenham itasikiliza ofa kwa ajili ya mlinzi wake wa kushoto wa Hispania Sergio Reguilon, 25, kufuatia tetesi za kutakiwa na klabu moja ya Hispania.

Crystal Palace wanamtaka kwa mkopo mlinzi wa Manchester United Aaron Wan-Bissaka. Nyota huyo mwenye miaka 24 ametokea kwenye kituo cha kukuza vipaji cha Palace na ameichezea Palace michezo 42.

Tetesi zinasema, Manchester United imekaribishwa kuwasilisha ofa kwa ajili ya kiungo wa Wolves mreno Ruben Neves, 25.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

West Ham na Aston Villa ni miongoni mwa timu zinazomuwania kumsajili kiungo wa Colombia James Rodriguez, 30, kutoka klabu ya Qatari, Al Rayyan.

Aberdeen imeiruhusu Leeds kuzungumza na kinda wa miaka 18 na mlinzi wake wa kulia Mscotland Calvin Ramsay.

Tetesi zinasema, Meneja wa Norwich Dean Smith anataka kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa Cameron Archer, 20 anayecheza kwa mkopo Preston.

Waamuzi wa ligi kuu England Martin Atkinson na Jonathan Moss watastaafu kuchezesha ligi hiyo mwishoni mwa msimu.


BURUDIKA NA KASINO BOMBA ZA MTANDAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa