Klabu ya Chelsea inamtazama mchezaji wa Villarreal, Pau Torres kama mbadala wa muda mrefu wa Antonio Rudiger anatarajiwa kujiunga na Real Madrid katika majira ya kiangazi.

Meneja wa Chelsea, Thomas Tuchel alithibitisha uamuzi wa Rudiger kuondoka klabuni hapo kutokana na mkataba wake kuisha lakini kushindwa kumuongeza mkataba mpya kutokana na marufuku iliyokwekwa dhidi ya mmiliki wa klabu hiyo Roman Abromovich.

 

chelsea, Chelsea : Torres Mbadala wa Rudiger., Meridianbet

Torres pia ananyatiwa na vilabu vya Manchester United, City na Tottenham lakini Blues ndio wanaoonekana kuwa na hamu zaidi kumsajili kutokana na kuelekea kupoteza mabeki wake wawili wa kati katika majira ya kiangazi.

Mbali na Rüdiger, ambaye tayari ana makubaliano na Real Madrid, Chelsea pia itampoteza Christensen, ambaye anatajwa kuelekea Barcelona.

Taarifa zinasema klabu hiyo ipo tayari kulipa kiasi cha karibu euro milioni 60 kwa klabu ya Villarreal ambayo ni kifungu kilichopo ili kuvunja mkataba wa beki huyo ili kupata huduma zake.


BURUDIKA NA KASINO BOMBA ZA MTANDAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa