Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah amechaguliwa kuwa mchezaji Bora wa mwaka wa Chama cha Waandishi wa Soka FWA kwa 2021/22.

Salah, 29, amechangia mabao 22 na asisti 13 katika michezo 31 ya Ligi Kuu ya Uingereza na kukisaidia kikosi hicho cha Jurgen Klopp kushika nafasi ya pili kwenye msimamo, alama moja nyuma ya mabingwa Man City zikiwa zimesalia mechi tano pekee msimu huu.

 

salah, Salah, Kerr Wachezaji Bora wa Mwaka FWA., Meridianbet

Wakati huo pia, mshambuliaji wa timu ya wanawake ya Chelsea, Sam Kerr amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Chama cha Waandishi wa Soka, FWA kwa 2021/22.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Australia kwa mara nyingine amekuwa kinara wa kikosi cha Emma Hayes, huku Fran Kirby na Pernille Harder wakiwa ndani na nje ya kikosi msimu mzima kutokana na majeraha.

Kerr ndiye mfungaji bora wa sasa katika Ligi kuu ya Wanawake akiwa amefunga mabao 18, likiwemo la goli la ushindi katika ushindi mgumu wa 2-1 dhidi ya Tottenham hapo jana.


 

BURUDIKA NA KASINO BOMBA ZA MTANDAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa