Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez amesema misimu miwili iliyopita katika Ligi ya Mabingwa Afrika hawakufanya vizuri kwenye mechi za ugenini, lakini msimu huu mambo yatakuwa tofauti.
Amesema katika kuhakikisha ugenini wanakuwa na matokeo mazuri pia wamesajili wachezaji wenye uwezo wa kwenda kuipigania timu huko tofauti na misimu miwili iliyopita kikosi hakifanani na sasa.

“Kama uongozi tumeongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji ambayo haikuwepo pindi tulipokuwa tunakwenda kucheza ugenini, lakini tumeajili wataalamu kama Culvin Mavunga (Video analystis) ili kuipa nguvu benchi la ufundi kwenye mechi za mashindano yote.
“Ukiangalia tumeboresha benchi la ufundi kwa kuwaleta watu wenye uwezo kama kocha mkuu, Didier Gomes, kocha wa makipa, mtaalamu wa mazoezi ya viungo ambaye anayetumia kifaa chenye (GPRS).
“Sayansi ambayo tunaitumia katika timu kwa wakati huu ni kubwa mno na teknolojia tunayoitumia inatusaidia sana na kuna baadhi ya mambo mengine ya msingi na mikakati ya kuona tunafanya vizuri zaidi katika timu msimu huu siwezi kuiweka wazi,” alisema Barbara.
Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.



Adelta
Yuko sahihi
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri sana
Khadija
yupo sahihi
Magdalena
Simba mchezo mzuri waliucheza
Sania
Simba kiboko yao
Rahmal
Safi sana simba nawaelewa sana
Dorophina
Tunasubilia kuona
Sarah
Yuko sawa kabisa
Hopemwaikuka
Itapendeza sana
samiah
Safi
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
warda
Tutapambana tu