Barcelona Kushtaki Gazeti la El Mundo.


Barcelona imesema kuwa itachukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti la Uhispania la El Mundo baada ya kuchapisha maelezo kuhusu mkataba wa mshambuliaji, Lionel Messi wa pauni milioni 492.

Barcelona ilikanusha kuhusika kwa namna yoyote ile katika uchapishaji wa taarifa hizo. Kwa mujibu wa El Mundo, mkataba wa Messi wa miaka minne ulikuwa wa thamani ya takriban euro 555,237,619 hadi Juni 30, 2021.

Hii inamaanisha kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, atakuwa anapokea pauni milioni 123 kwa msimu.

 

Timu hiyo imesema katika taarifa iliyotoa kuwa inasikitishwa na uchapishaji wa maelezo hayo. Na kuongeza kuwa: “FC Barcelona haihusiki kwa namna yoyote ile katika uchapishaji wa taarifa hiyo na itachukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya gazeti la El Mundo, kwa uharibifu wowote ule ambao huenda umetokea kwasababu ya taarifa hiyo.

FC Barcelona imeonesha kumuunga mkono Lionel Messi, hasa katika jaribio lolote la kumdhalilisha na kuharibu uhusiano wake katika klabu hiyo ambako amefanyakazi na kuwa mchezaji bora duniani na katika historia ya soka.”

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina Messi alijiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 13 lakini akatuma ombi la kutaka aruhusiwe kuhamia kwingineko mnamo mwezi Agosti.


Tungeneza Faida KUPITIA Kasino ya Meridianbet

Neptune’s Richies ni mchezo Unaokupa pesa chap chap huku ukiwa unaburudika kupitia Kasino ya Mtandaoni ndani ya Meridianbet.

Neptune's-Riches_Casino-Post_30-January

Cheza hapa

12 Komentara

    Duh hiyo balaa sasa

    Jibu

    Hii ni makala yenye maelezo mazuri kwa kutuelimisha sisi mashabiki tusubiri tuone itakuwaje

    Jibu

    Duuh atariii sana

    Jibu

    Mbona hatariii

    Jibu

    Ni balaa

    Jibu

    Kama barca wanakataa aliyechapisha kazeti hilo atafutwe hili kuliweka hili sawa

    Jibu

    Mbona baraha zito

    Jibu

    Hatari sana

    Jibu

    Vzur maana wanazd

    Jibu

    Nushidaaa

    Jibu

    Acha washitakiane mana mambo ya pesa hayo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.