Miamba ya kandanda ya Ujerumani Bayern Munich na Borussia Dortmund ziliangukia pua mwishoni mwa wiki katika mechi zao za ligi kuu Bundesliga lakini wana fursa ya kurejea tena haraka kwenye mkondo wa ushindi.
Itakutana kwa mara ya kwanza msimu huu siku ya Jumatano dimbani Allianz Arena katika fainali ya DFL Super Cup. Washindi wa mataji mawili makuu ya nyumbani Bayern watawaalika Dortmund ambao ni makamu bingwa wa Bundesliga, kujaribu kubeba taji lao la tano katika mwaka wa 2020.

Baada ya mechi 32 za ushindani bila kushindwa, ukiwemo ushindi wa mechi 23 za mwisho, Bayern walionja kichapo kizito cha 4 – 1 mikononi mwa Hoffenheim.
Walicheza saa 48 tu baada ya kurejea kutoka Budapest, ambako walibeba taji lao la nne katika mwaka mmoja la UEFA Super Cup dhidi ya Sevilla, ushindi uliopatikana katika muda wa nyogeza.
Kocha wa Bayern Munich Hansi Flick amekataa kutoa sababu ya uchovu wala kuwalaumu wachezaji wake kwa kipigo hicho maoni ambayo yanaungwa mkono na Thomas Müller.

Ni wazi kuwa ingefika siku ambayo unapoteza mechi nyingine. Nadhani tulikuwa pia na nafasi moja au mbili ambazo tungeweza kurekebisha. Lakini kwa dakika 90 hatukustahili kutoka sare au hata kushinda mchezo. Hoffenheim ilifanya kazi nzuri leo. Kwa mukhtasari, tulistahili kushindwa na tutarudi Jumatano.
Macho yote yataelekezwa katika Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa mvutano, pamoja na kuwakosa wachezaji wawili wakariba ya juu, Jadon Sancho na Thiago Alcantara aliyejiunga na Liverpool.
Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!
Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!


Elika
Dortimund kama kawaida yao lazima kichapo kitembee kwa munich
magdalena
apo kazi ipo sizani kama bayern munich atakubali kupokea kichapo nyumbani kwake
Mwajumah
Mmh hii mechi itakua ya kukata na shoka maana Kila mtu anataka kutetea upande wake
Adelta
Leo kazi ipo tusubiri tuone matokeo
Sauda
Bayern lazima achukue ubingwa.
Nasra
Dortmund nawakubali
Fatina mfigi
Leo ndo leo pamban litakuwa kali!!
Zeiyana
Dortmund wajiandae kile kichapo walichopigwa nne Bayern asila zote watamalizia kwao kama wasipo jipanga wanaweza kupata haibu ya mwaka leo
Dorophina
Dortmund lazima akiwashe
Venerose
Wote wapo vinzur itakuwa big game
Caroline
Mbona wameanza vibaya
Latifa juma mohamed
Daah hii mechi ya kukata na shoka maana timu zote zipo mstari wa mbele.
Hopemwaikuka
Dk 90 zitatoa majibu
Sadick
Mechi ngumu kwa kila timu, ningependa kuona Dortmund ikishinda kuleta ushindani#meridianbettz
Shani
Dortmund watakaa tu kwenye hii mechi Munich wapo vizur kombineshen ya gnarbry na lewandoski ni moto
Johnmary joel
Mpira ulikuwa wa hatari sana #meridianbett
aisha
Bayern wanauchung wakufungw
Hidaya
Dk 90 ndio muamuzi
Khadija
Mpira dk90
Saupha mohamed
Tusubili matokeo
Issa
Ni mechi ngumu sana tutashuhudia upinzan wa haaland na lewandoski
Fatuma kasomo
Kazi ipo hapo
Gabriel
Hii n bonge la mechi kal sana 👍
Amiri Kayera
Bonge la mechi ambay nashindwag kujua nan atashinda
Sabrina
Mi nasubiri matokeo tu maana nina mkeka wangu unapumua
Rehema
Safi
felister
sijui matokeo yalikuaje ya hii mechi…?
Lydia Emmanuel Magoti
Naisi ilikuwa apatoshi sio kwamechi hizo nazo ziona palikuwa apatoshi mtanange huo
Tatu
Ngoma ngumu hii
Neema
Dakika za mwishoo tutajua mbabee wao
Ernest
Kocha kwa Dortmund alibugi sana kumfanyia sub Haaland mapema baada ya kusawazisha goli la pili
Mwanahamisi
Tusubili matokeo
David Pere
apo kazi ipo sizani kama bayern munich atakubali kupokea kichapo nyumbani kwake
Samiah
Tusubiri tuone matokeo