Chelsea Yapata Ushindi wa Kwanza UEFA

Klabu ya Chelsea imepata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya hapo jana walipokuwa nyumbani kwake, baada ya mchezo wake wa kwanza kufungwa na wa pili kutoa sare.

 

Chelsea Yapata Ushindi wa Kwanza UEFA

Chelsea ambayo kwasasa ipo chini ya kocha mkuu Graham Potter ilimgalagaza AC Milan mabao 3-0, mabao hayo yalitupiwa wavuni na Wesley Fofana, Aubameyang pamoja na Recce James.

Timu hiyo mpaka sasa kwenye kundi E ipo nafasi ya pili ikiwa na alama nne ambazo ni sawa na za Milan ila tofauti yao kubwa ikiwa ni magoli ya kufunga na kufungwa. Kwa kocha nae huo unakuwa ushindi wake wa pili toka ajiunge na klabu hiyo ambapo mchezo wa kwanza kushinda ni wa kwenye ligi kuu ya Uingereza.

Chelsea Yapata Ushindi wa Kwanza UEFA

Mechi ijayo kwenye Klabu Bingwa The Blues watakuwa ugenini kwa Milan, baada ya kucheza na Wolverhampton kwenye mchezo wa ligi kuu. Huku Milan akitaka kulipa kisasi na wakati huo Potter akitaka kuendeleza ubabe.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.