Xabi Alonso Kocha Mpya Leverkusen.

Gwiji wa zamani wa vilabu vya Real Sociedad,Liverpool,Real Madrid, Bayern Munich na timu ya taifa ya Hispania Xabi Alonso amechaguliwa rasmi kua kocha wa klabu ya Bayern Leverkusen ya nchini Ujerumani.

xabi alonsoXabi Alonso amechaguliwa kua kocha wa klabu hiyo kuchukua nafasi ya Gerardo Seoane baada ya Leverkusen kumfuta kazi kocha huyo na kumtangaza gwiji huyo wa zamani wa Real Madrid. Alonso ambaye alikua akifundisha timu B ya klabu yake ya zamani ya Real Sociedad.

Kocha huyo mpya wa Bayern Leverkusen pia amewahi kufundisha klabu ya Real Madrid ya vijana chini ya miaka 14 kabla ya kwenda kufundisha Real Sociedad B, Kocha huyo anatarajiwa kua mwalimu mzuri kutoka na kupita chini ya walimu bora wakati anacheza na makocha hao ni kama Carlo Anchelotti, Pep Guardiola,Jose Mourinho na Rapha Benitez.

xabi alonsoXabi Alonso wakati wa uchezaji wake kama kiungo amefanikiwa kubeba karibu mataji yote aliyowahi kugombania kama mchezaji mataji ligi ya mabingwa ulaya 2, kombe la dunia mara moja,kombe la mataifa ya ulaya mara moja pamoja na mataji mengine mengi ya ndani katika timu tofauti alizopita.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.