Klabu ya soka ya Sevilla inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Hispania imemtimua kocha wake mkuu Julien Lopetegui baada ya matakeo yasiyoridhisha ya klabu hiyo siku za karibuni.
Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Real Madrid amefukuzwa kazi baada ya matokeo ya jana katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu ya Borussia Dortmund,baada ya kupigwa magoli manne kwa moja katika uwanja wao wa nyumbani wa Ramon Sanchez Pizjuan, jambo lililowafanya mabosi wa Sevilla kushindwa kuvumilia hali hiyo ikiwa ni pamoja na klabu hiyo kufanya vibaya msimu huu kwenye michuano hiyo.
Sevilla baada ya michezo mitatu ya ligi ya mabingwa ulaya wameambulia alama moja huku wakifungwa michezo miwili na kupata sare mchezo mmoja jambo ambalo limefanya klabu kufanya mabadiliko ya mwalimu haraka ili kuinususru timu hiyo mapema.
Kocha Lopetegui inakua mara ya tatu kufukuzwa baada ya kufukuzwa timu ya taifa ya Hispania,Real Madrid pamoja na sasa ndani ya mabingwa hao mara tatu mfululizo wa zamani wa Uefa Europa League.

