Potter: James Anaweza Kuwa Gwiji wa Chelsea

Kocha mkuu wa Chelsea Graham Potter anaamini kuwa beki wake wa pembeni Reece James ana sifa zote za kuwa “gwiji” wa Chelsea baada ya kuwa na ubora msimu huu pamoja na kuifanikisha timu yake kupata alama tatu hapo jana.

 

Potter: James Anaweza Kuwa Gwiji wa Chelsea

James alitoa assist kwa  Pierre-Emerick Aubameyang kwa bao la pili la Chelsea kufuatia Wesley Fofana kufunga bao la kwanza, kabla ya kupata majeraha na kutolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Trevoh Chalobah.

Fofana hilo lilikuwa bao lake la kwanza toka ajiunge na klabu hiyo kutoka Leicester City, huku akitolewa nje kufuatia kupata jeraha kwenye goti. Potter amesema kuwa hana uhakika na ukali wa jeraha lake na amesema kuwa kijana huyo mwenye umri wa miaka 21 atafanyiwa uchunguzi siku ya Alhamisi.

Potter: James Anaweza Kuwa Gwiji wa Chelsea

Reece James akiwa na  miaka 22 na siku 301, alikua mchezaji mdogo zaidi wa Chelsea kufunga na kusaidia bao katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa, na kumvutia Potter na kusema kuwa beki huyo atakuwa ni moja ya magwiji wa klabu hiyo.

“Nadhani Reece ni mchezaji mzuri tu na ni mchezaji mchanga,” Potter alisema katika mkutano na waandishi wa habari. “Anakua kila wakati; atakuwa bora na bora tunapoenda.

Potter: James Anaweza Kuwa Gwiji wa Chelsea

Potter anasema amefurahishwa na kazi yake kwani ana mengi ya kutoa klabuni hapo, Aliongezea kuwa James anaweza kucheza katika mchezo wowote Duniani na ni muhimu sana kwa kikosi chake na kazi yake ni kumsaidia kufikia uwezo wa kuwa gwiji wa Chelsea.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.