Makamu mwenyekiti wa klabu ya Juventus Pavel Nedved amesema hawana shaka na kocha wa klabu hiyo kwakua wanaamini katika ubora wa kocha huyo.
Juventus ambao wameanza vibaya msimu huu wa 2022/23 kwenye ligi ya nyumbani ya Serie A pia katika ligi ya mabingwa ulaya huku wakipoteza mechi mbili za awali katika kundi H kabla ya kushinda mchezo wa jana dhidi ya Maccabi Haifa kitu kilichofanya mashabiki wa klabu hiyo kudhani ni muda sahihi wa kuachana na Allegri.
Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Pavel Nedved bado ameendelea kusisitiza hatama ya kocha wa klabu hiyo haipo mashakani kabisa “Tunafanya kila kitu, klabu,kocha, wafanyakazi, ili kuturudisha kwenye mstari, kucheza kama Juve ili kufuzu raundi inayofuata na kurudi kwenye ushindani kwenye Serie A”Alisema Pavel
“Hatujawahi kua na shaka na kocha hata kidogo, nataka niweke wazi” Aliiambia skysport Italy bwana Pavel Nedved akiendelea kuonesha namna timu hiyo inamuunga mkono kocha wao na wana mipango nae mikubwa ya mbeleni.
Massimiliano Allegri alichukua nafasi ya gwiji Andrea Pirlo baada ya kuondolewa klabuni hapo baada ya matokeo mabaya lakini hali inaonekana bado kutobadilika baada ya Allegri kurejea klabuni hapo mara ya pili.

