Kiungo wa klabu ya West Ham United na timu ya taifa ya Uingereza Declan Rice amewekwa sokoni rasmi na klabu yake baada ya kauli ya mwenyekiti wa klabu ya David Sullivan ambayo ameitoa.
Mwenyekiti wa klabu ya West Ham David Sullivan amesema kua kiungo Declan Rice amecheza mchezo wa mwisho na klabu hiyo siku ya jana katika fainali ya Uefa Conference League, Huku akikaribisha timu ambazo zinamtaka kiungo huyo mezani kwajili ya kufanya mazungumzo ya kumuachia.
Klabu ya Arsenal bado inaongoza katika mbio za kumuwania kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza wakiamini kama mbadala sahihi wa mchezaji Thomas Partey, Lakini kuna vilabu vingine ambavyo vinavizia saini ya kiungo huyo lakini washika mitutu wa London bado wako mbele kwenye mbio hizo.
Kiungo Declan Rice amekua kwenye kiwango bora sana kwa misimu takribani mitatu ambayo ameitumikia klabu hiyo, Huku klabu ya Fc Bayern Munich kutoka nchini Ujerumani nayo inaelezwa kuhitaji huduma ya kiungo huyo mwenye thamani kubwa kwasasa katika ligi kuu ya Uingereza.
Declan Rice amekua akihusishwa pia na mashetani wekundu klabu ya Manchester United japo Arsenal wanaelezwa kua mbele kwenye mbio hizo, Washika mitutu kutoka jiji la London inaelezwa wameshaandaa ofa yao tangu mwezi wa tano hivo ni suala la kuwasilisha ofa yao kwa klabu ya West Ham.

