Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Hassan Dilunga, amekabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa Oktoba wa mashabiki (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month) na wadhamini Emirate Aluminium ACP.
Dilunga (2249) amewapiku viungo wenzake Rally Bwalya (2199) na Sadio Kanoute (376) ambao waliingia fainali ya kinyangβanyiro hicho. Emirate imemkabidhi kitita cha Sh 2,000,000 na ngao kama sehemu ya zawadi baada ya kunyakua tuzo hiyo.
Meneja Masoko na Mahusiano wa Emirate Aluminium ACP, Issa Maeda amesema ni tuzo kubwa ambayo inatolewa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati na haijawahi kutolewa kabla.
βEmirate Aluminium ACP tunatoa kiasi kikubwa cha fedha kwa mchezaji bora wa Simba, ni kikubwa mara mbili zaidi ya msimu uliopita, hata mchezaji bora wa ligi hapati kama hiki nadhani itaongeza chachu kwa wachezaji kuendelea kufanya vizuri,β amesema Maeda.
Kwa upande wake Dilunga amewashukuru mashabiki kwa kumpigia kura nyingi na wamemfanya kujiona ana deni kubwa na ataendelea kujituma kama sehemu ya kurejesha shukrani kwao.
βKwanza nawashukuru mashabiki kwa kunipigia kura nyingi, naishukuru familia yangu na marafiki wa karibu kwa kuhamasisha mpaka nikapata tuzo hii, kiukweli najiona nina deni kubwa na nitaendelea kupambana kupata tena na tena,β amesema Dilunga.
Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.