Alonso Aisifu Leverkusen kwa Kuweka Rekodi Yao Jana

Kocha mkuu wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso ameipongeza timu yake kwa kuweka rekodi yao hapo jana baada ya kupata ushindi mnono kwa kuichabanga Union Berlin mabao 5-0.

 

Alonso Aisifu Leverkusen kwa Kuweka Rekodi Yao Jana

Kikosi cha Mhispania huyo kilikabiliwa na mtihani mgumu dhidi ya Union katika uwanja wa BayArena, huku wageni hao wakijua ushindi ungewafanya kurejea kileleni mwa Bundesliga mbele ya Bayern Munich.

Baada ya kipindi cha kwanza kisicho na bao, Robert Andrich alifunga bao dakika moja baada ya kuanza tena kipindi cha pili na ushindi  huo ulikuwa ushindi wa juu zaidi kwa timu ya Bundesliga kwenye milenia hii huku ni Bayern tu ambaye aliweza kumfunga Dortmund mabao 5-0 mnamo April 2019.

Alonso Aisifu Leverkusen kwa Kuweka Rekodi Yao Jana

Ushindi huo kwa Leverkusen ulikuwa muhimu sana kutokana na kupigwa mechi sita mfululizo bila kushinda katika michuano yote na ikawa ushindi wa tatu pekee wa ligi kwa Leverkusen msimu huu, na kumfanya Alonso kusifu uchezaji wa timu yake.

Alonso alisema kuwa “Kipindi cha kwanza hakuna aliyepata nafasi nyingi na haikuwa rahisi kushambulia. Union wanasimama juu sana kwenye msimamo kwasababu fulani”

Kipindi cha pili wakazidisha uimara na wakapata nafasi nyingi zaidi, huku wachezaji wao wenye kasi wakikimbia sana na walikuwa wazuri sana kumalizia mpira kambani na wana furaha sana kwasababu ya ushindi huo, na wanataka kuendelea hivyo hivyo.

Alonso Aisifu Leverkusen kwa Kuweka Rekodi Yao Jana

Kikosi cha Alonso sasa kina mechi mbili za Bundesliga dhidi ya Koln na Stuttgart kabla ya Kombe la Dunia nchini Qatar, huku kampeni ya ligi hiyo ikitarajiwa kurejea Januari 22, ambapo mpaka sasa wanashikilia nafasi ya 14 wakiwa na pointi 12 tu.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

Acha ujumbe