Bayern Munich Wamethibitisha Kuwa Wako Kwenye Mazungumzo ya Kuongeza Mkataba wa Kane.

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich, Max Eberl, Jumatatu alithibitisha kuwa klabu iko kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba wa Harry Kane. Mshambuliaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 32, aliyejiunga na Bayern mwaka 2023, ana mkataba unaoendelea hadi mwaka 2027.

Bayern Munich Wamethibitisha Kuwa Wako Kwenye Mazungumzo ya Kuongeza Mkataba wa Kane.

“Tunaongea na Harry, mazungumzo yanaendelea,” Eberl alisema wakati wa tukio la Bundesliga mjini Frankfurt. “Kila mtu anajua kuwa kufikia wakati fulani uamuzi lazima ufanywe,” aliongeza.

Mkurugenzi Mtendaji wa klabu, Jan-Christian Dreesen, pia alisema Harry ana imani kubwa nao na anajisikia vizuri sana akiwa Munich. Yeye na familia yake wameshazoea mazingira, hivyo hawana sababu yoyote ya kuharakisha.

Baada ya muda mrefu bila kutwaa taji la timu, Kane alivunja ukame huo mwaka 2025 pale Bayern walipotwaa ubingwa wa Bundesliga.

Msimu huu, Bayern wako mbele kwa pointi nane kileleni mwa ligi na wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya yenye timu 36.

Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.

Bayern Munich Wamethibitisha Kuwa Wako Kwenye Mazungumzo ya Kuongeza Mkataba wa Kane.

Akizungumza Oktoba, Kane alisema anaweza “kuona kabisa” uwezekano wa kuongeza muda wa kukaa kwake nchini Ujerumani.

Kane amefunga mabao 119 katika mechi 126 alizocheza akiwa Bayern, pamoja na kutoa pasi za mabao 30. Msimu huu pekee, ana mabao 34 katika mechi 30. Akiwa na mabao 21 katika mechi 19 za Bundesliga, Kane yuko kwenye mwelekeo wa kuvunja rekodi ya mabao mengi kwa msimu mmoja (41) iliyowekwa na Robert Lewandowski msimu wa 2020–21.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.