Bayern Munich imeonyesha ubora wake kwa kuibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Flamengo, na kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia la Klabu. Katika mchezo wa kusisimua uliovuta hisia za mashabiki zaidi ya 60,000 kwenye Uwanja wa Hard Rock Stadium. Nyota wa mchezo alikuwa mshambuliaji mahiri Harry Kane, aliyefunga mabao mawili na kuiongoza Bayern dhidi ya wapinzani kutoka Amerika Kusini.

Mchezo ulianza kwa kasi huku Bayern wakionyesha makali yao mapema kabisa. Joshua Kimmich aliwafungulia njia katika dakika ya 6 kabla Harry Kane kupachika bao la pili dakika ya 10, na kufanya mchezo uonekane kama utamalizika mapema.
Hata hivyo, Flamengo, mabingwa mara tatu wa Copa Libertadores, walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Gerson aliyemalizia pasi ya Luiz Araujo dakika ya 33, na kuamsha matumaini kwa upande wa Brazil. Lakini matumaini hayo yalipotea dakika ya 41 baada ya makosa ya Araujo kumruhusu Leon Goretzka kutuliza mpira na kupiga shuti la umbali wa zaidi ya yadi 20 lililompita kipa Agustin Rossi, na kufanya matokeo kuwa 3-1 hadi mapumziko.

Kipindi cha pili Flamengo walirejea kwa ari na walizawadiwa penalti dakika ya 55 baada ya mpira wa kona kugonga mkono wa Michael Olise. Jorginho hakufanya makosa na kuipatia Flamengo bao la pili, na hivyo kuweka presha upya kwa Bayern.
Licha ya juhudi hizo, ubora wa Bayern ulijidhihirisha tena dakika ya 73 kupitia harakati nzuri kutoka kwa Konrad Laimer aliyepokonya mpira katikati ya uwanja na kumchezesha Kimmich, ambaye alimpa Harry Kane pasi murua. Kane alimalizia kwa utulivu na kuhitimisha ushindi kwa bao la nne.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha wa Flamengo, Filipe Luis, baada ya mchezo alikiri ubora wa wapinzani wake kwa kusema, “Watawala wa soka bado wako Ulaya.” Kauli inayothibitisha vilabu vya Ulaya kutawala mashindano ya Dunia.
Sasa, kikosi cha Vincent Kompany kitaumana na Paris Saint-Germain siku ya Jumamosi huko Atlanta kutafuta nafasi ya kutinga nusu fainali. Hii itakuwa mechi ya kusisimua kati ya vigogo wawili wa soka la bara Ulaya.


