Cole Kuungana na Lampard

Cole [38] anaonekana kutaka kuungana na mchezaji mwenzake wa kipindi cha nyuma Lampard katika klabu ya Chelsea. Wachezaji hao waliachana kwa kitambo kidogo baada ya kustaafu soka la ushindani pale Uingereza na ndipo Lampard akabahatika kupewa timu ya kuiongoza nchini Uingereza, Derby huku rafiki yake akiwa bado mchezaji huko Marekani. Alikuwa akikipiga na LA Galaxy lakini kwa sasa anekuwa mchezaji huru baada ya kutemana na miamba hao; kitu kinachomfanya kuwa mchezaji huru kwa sasa.

Mazungumzo ya awali bado yanaendelea na yanaonekana kutoka na majibu mazuri hapo baadae maana yanaushawishi wa kumwona mvhezaji huyo akitua ndani ya kikosi hicho kwa siku za mbeleni. Hivyo, hali iliyopo ni kwamba maridhiano hayo yanaweza kutoa mwafaka muda wowote kuanzia sasa hadi baadae juu ya taarifa hiyo.

Katika mazingira ya kawaida ya uwanjani Cole atakuwa msaada ndani ya timu hiyo kama wasemi wasemavyo ‘Kijiwe bila wazee sio kijiwe’ hivyo ana kila jambo la pekee kuwaeleza na kuwamwagia madini wachezaji wa Derby na kuamsha ari ya kujituma. Akiwa amecheza michezo zaidi ya 100 ndani ya Uingereza kati ya 2001 hadi 2014. Na katika ngazi nyingime amefanikiwa kucheza mechi zaidi ya 650

Ana historia yake baada ya kunyanyua kombe la ligi na lile la klabu bingwa barani Ulaya akiwa na Arsenal, pia akiwa kama mchezaji wa Arsenal aliwahi kuchangia sehemu ya maajabu ndani ya klabu hiyo kwa kuweza kushinda mechi 49 bila kuachia mechi hata moja, historia hiyo iliandikwa miaka ya 2003/4.

Lampard yeye anakiri kwamba hadi sasa hajafanya mawasiliano yoyote na rafiki yake huyo wa kitambo lakini, aligasikia haya na alihisi yangetokea mapema sana. Na haoni ugumu wowote juu ya kufanya kazi kama hizi za kuwasiliana na watu ambao ameweza kuwa nao kwa namna moja au nyingine. Hivyo haoni ugumu wowote na kwake suala hilo ni rahisi sana kuliweka sawa kama itakuwa na ukweli juu ya hilo.

Ronaldo aliwahi kumzungumzia mchezaji huyo kuwa ni wa aina yake kutokana na uwezo wake wa kuwazuia wapinzani wake kuweza kupenya uwanjani hasa kupitia upande wake. Ni aina ya mabeki ambao wana akili na nguvu kuweza kumkata kabisa nguvu mchezaji yeyote anayetaka kuivamia ngome yake.

Jadi meo anabaki katika kichwa cha Ronaldo kwamba ni aina ya mabeki ambao wamemtesa na kumsumbua sana katika maisha yake ya soka kutokana na kumpa upinzani mzito ambao kwa wakati mwingine ulimkasirisha sana anapotafuta matokeo, na hadi leo anabaki kuwa mwoga kukutana na walinzj wa aina yake.

3 Komentara

    Lampard snajua sana.

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    asante kwa taarifa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.