Tetesi: Rashford Kusaini Dili Zito Trafford!

Mchezaji huyo kwa sasa amefanikiwa kubadilika kwa kiwango kikubwa sana tofauti na alivyokuwa mwanzoni, pongezi nyingi zimfikie  Ole ambaye kwa nafasi yake anefanikiwa kymtengeneza na amejua namna ya kumtumia mvhezaji huyo ndani ya uwanja kwa utofauti mkubwa sana na nyakati za nyuma.

Kwa kipindi kirefu amehangaika kwa namna moja au nyingine kuendana na baadhi ya falsafa na mifumo ya mwalimu wake wa awali. Tangu alipoifungia timu hiyo katika hatua ya Europa walipocheza na FC Midtjylland alionekana kupotea kabisa kwa kiwango kikubwa hadi sass katika kipindi huki anaonekana tegemezi ndani ya kikosi hicho.

Mazingira yalikokuwa yanaendelea chini ya mchezaji huyo ilikuwa ni kukosa kabisa nafasi ya kucheza kikosini hapo pamoja na ubora wake; lakini punde si punde baada ya meza kupinduliwa mambo yakaanza kwenda vizuri kwa mchezaji huyo kutokana na kupata namba kikosini hapo na kuaminiwa makubwa anayoyafanya ndani ya klabu hiyo.

Mourinho alikosa imani kabisa na mchezaji huyo hadi kutaka kumtoa kwa mkopo ili aweze kukua kisoka, kitu ambacho kisingeweza kukubaliwa kikosini hapo kwa namna yoyote ile. Maamzi yaliyofikiwa ni hayo ya kumwondoa kocha ili waweze kuondoa baadhi ya kauli zilizokuwa zinakinzana na matakwa ya klabu.

Matajiri hao kwa sasa wanategemea kumpa mcjezaji huyo kitita cha kuridhisha kwa kutambua kile kitakachofuta jina hilo kwa klabu nyingine zinazoonesha nia ya kumvizia mshambuliaji huyo. Atajuwa analipwa kiasi cha £150k ambayo itakuwa mara mbili ya ile anayopokea sasa ambayo ni £75,000, hiyo ni hatua chanya kwa mchezaji huyo.

Kandarasi yake ya sasa itafikia ukomo 2020, lakini ndani ya kanuni za kandarasi iliyopo; klabu ina machagulio ya kumwongeza mkataba mwingine kwa mshahara uleule. Lakini klabu hiyo inawiwa kumwongezea kandarasi nyingine ambayo itakuwa na malipo ya mara mbili zaidi ya kile alichokuwa anapokea awali.

Ndoto za Juventus na Real Madrid kwa sasa itabidi ziweze kuyeyuka kutokana na aina ya kandarasi anayotegemewa kuisaini mchezaji huyo ndani ya viwanja hivyo, kwani anaomekana tayari ameridhika sahihi kabisa na mazingira yale.

Endapo atacheza mechi dhidi ya Brighton atakuwa anatimiza mechi yake ya 150 katika ligi hiyo, chini ya klabu hiyo kitu ambacho ni hatua kubwa kwake ikifananishwa na umri wake ambao bado ana mengi makubwa ya kufanya.

Na endapo atafanikiwa kufunga pia katika mechi hiyo kwa sasa atakuwa ameandika histoia mpya ndani ya klabu hiyo na utawala mzima ndani ya klabu hiyo.

 

3 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Namkubali sana.

    Jibu

    Good

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.