Balloteli Kuendelea Kusakata Kabumbu

Mchezaji huyo amekuwa picha la kutisha katika ligi mbalimbali duniani kwa kupitia kampeni zake za kupinga ubaguzi na kupambana juu ya kupata namba ya kudumu ndani ya kikosi hicho cha klabu hiyo. Kwa sasa anakipiga katika klabu ya Nice ambako anatumikia salama kabisa bila shida ambazo kipindi cha nyuma alionekana kuzifanya, hadi kuanza kuonrkana kama hana faida kabisa kutokana na kesi nyingi za utovu wa nidhamu kwa kupigana au kutukana waamuzi.

Kuna wakati unaweza unaweza kufikiri kwamba mchezaji huyo ameweza kuzunguka katika klabu nyingi sana kuliko kawaida lakini ndivyo sivyo, amepitia klabu sita tu hadi sasa kitu ambacho ni cha kawaida sana katika soka. Akiweza kuichezea AC Milan mara mbili katika historia yake ikihusishwa na ile aliyokuwa chipukizi wa miaka 19 katika kikosi hicho.

Kutokana na kuhusishwa na kuhama klabu zake mara nyingi katika mzingira ya kawaida inaweza onekana kama amegusa kila aina ya ligi duniani lakini ni kwa namna tu anavyohusishwa na klabu nyingi mara kadhaa, kitu kinachodhaniwa yaweza kuwa ule utukutu wake mara kadhaa akiwa kwenye klabu anazopitia.

Akiwa Nice ndani ya miaka miwili alijaribu kutulia na kuonekana kama aina fulani ya wachezaji ambao klabu hiyo inawataka, huku akiweza kufumania nyavu mara 43 katika michezo 66 aliyocheza na klabu hiyo. Hicho ndicho kipindi ambacho alionekana kutulia katima maisha yake ya soka ikilinganishwa na aliyoyafanya kipindi cha nyuma.

Kutokana na kashkashi hizo msimu huu alionekana kutaka kujiunga na Marseille kwa kulazimisha uhamisho wake lakini kwa bahati mbaya hakuweza kufanikiwa katika hilo kutokana na kuchelewa kuanza kulifuatilia suala hilo kwa wakati ule. Japo anaweza kutimkia huko kwa uhamisho huru katika kipondi cha hivi karibuni baada ya uke wa mwanzo kufeli. Lakini hadi sasa mkataba wake umesalia yapata miezi miwili tu, kitu kinachoweza kuharakisha kuondoka klabuni hapo.

Mchezaji huyo aliyewahi kuichezea Manchester City hajawa ndani ya uwanja tangu 4, Disemba na akitimka klabuni hapo atakuwa anapokea kiasi cha €2M katika klabu yake mpya atakayojiunga nayo upya. Pamoja na mwanzo mzuri ndani ya klabu hiyo, ameshindwa kabisa kufunga katika mechi zake 10 alizozicheza na klabu hiyo ya Nice hadi sasa.

Anatuachia ule msemo wa ‘Mwanzo mwema, mwisho mbaya’ kwa namna alivyoweza kutumikia ndani ya klabu hiyo kwa kuanza kwa kasi nzuri lakini mwisho wake umekuja kumwangusha kwa kupotea kabisa kama mfungaji mkubwa na tegemezi katika kikosi hicho anachotumikia kwa sasa. Ana nafasi kubwa ya kuendelea kufanya vizuri katika klabu yake mpya anayotegemea kujiunga nayo kwa sababu umri wake bado unamruhusu na kushawishi yeye kufanya hivyo.

 

Β 

2 Komentara

    Anatuachia ule msemo wa β€˜Mwanzo mwema, mwisho mbaya’ kwa namna alivyoweza kutumikia ndani ya klabu hiyo kwa kuanza kwa kasi nzuri lakini mwisho wake umekuja kumwangusha kwa kupotea kabisa kama mfungaji mkubwa na tegemezi katika kikosi hicho

    Jibu

    Balotel n mchezaji mzur tatizo lake n ujeur tu ndo maana unfanya kuogopwa na baadhi ya club kumsajil ila n mchezaji mzur tena sana na anapiga mpira kwa level ya juu kabisa
    # meridianBetTZ

    Jibu

Acha ujumbe