Fellaini Kusalia Manchester United

Mchezaji Marouane Feallain ambaye ni kiungo wa klabu ya soka ya Manchester United ameongeza mkataba wake kwa muda wa miaka miwili ili kuendelea kucheza klabuni hapo.

Hapo mwanzo ilielezwa kuwa Mbeligiji huyo ataondoka Manchester United ila mambo yamekuwa tofauti na kiungo huyo ameongeza mkataba zaidi!

Huu mkataba wa United na Fellaini utamalizika ifikapo mwaka 2020 ikiwa ni mara baada ya wao kukubaliana na uongozi wa Manchester United ikiwemo hitaji la kocha wao.

Mpaka sasa Fellain ameifungia klabu ya United jumla ya magoli 20 kwenye mitanange 156 ambayo ameitumikia klabu hiyo ya Uingereza.

Mara baada ya yeye kusaini mkataba amefunguka na kuweka wazi kuwa anafurahia sana kuendelea kubakia United na hii ni kutokana na furaha aliyonayo awapo klabuni hapo.

3 Komentara

    Safi

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

Acha ujumbe