Kocha mkuu wa PSG, Christophe Galtier alisisitiza kwamba Kylian Mbappe ana furaha akiwa Paris Saint-Germain, ingawa alikiri mustakabali wa Lionel Messi na wababe hao wa Ufaransa haujaamuliwa.

Mbappe ndiye mchezaji anayeongoza katika Ligue 1 msimu huu akiwa na magoli 12 mbele akimzidi mchezaji mwenzake Neymar wakati Messi anaongeza chati akiwa na assist 10, pia baada ya kuchana wavu mara saba.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ufaransa alihusishwa pakubwa na uhamisho wa bila malipo kwenda Real Madrid msimu uliopita, lakini hatimaye alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu na mabingwa hao watetezi wa Ligue 1 mwezi Mei.
Wengi waliamini kuwa faida ya kifedha ilichangia sana uamuzi wa Mbappe, huku ripoti zikisema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 hivi majuzi amekuwa akifikiria upya iwapo anataka kubaki katika klabu hiyo.

Lakini Galtier aliiambia Marca: “Sidhani kama pesa hizo, kwa sababu wachezaji wa kiwango cha Kimataifa iwe Hispania, Uingereza au Ufaransa wanazishinda, na si kwa ajili ya pesa hizo. Nafikiri Kylian anaipenda tu PSG.”
Galtier aliongeza kuwa ikiwa ana furaha, kwanini Kylian asiwe hapa msimu wa joto? Kuanzia wakati mchezaji anafurahia uwanjani na kuhisi kwamba yuko kwenye timu ambayo inaweza kushinda na ambayo inaweza kushinda changamoto kubwa, hana sababu ya kuondoka.
Alipoulizwa kama anahisi Mbappe alikuwa na furaha PSG, Galtier aliongeza na kusema kuwa ndiyo, hakika imehakikishwa, wakati huo huo mkataba uliopo wa Messi unatarajiwa kumalizika Juni ijayo, ingawa kuna chaguo la kuongeza muda wake wa kukaa katika mji mkuu wa Ufaransa kwa mwaka zaidi.

Mchezaji ili abakie ndani ya timu, jambo la kwanza ni hamu yake. Unataka kuendelea PSG? Je, una furaha hapa? Jambo la kwanza kujua ni kama anataka kuendelea. Maamuzi ya aina zote hizi hufanywa kati ya mchezaji na mshauri wa soka Luis Campos.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.
BONYEZA HAPA KUCHEZA


