Foden, Trent Wazua Gumzo

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza Phil Foden na Trent Alexender Arnnold wamezua gumzo kwa mashabiki wa timu ya taifa ya Uingereza baada ya kuwekwa benchi kwa wachezaji hao.

Mashabiki wengi wa timu hiyo wakiongozwa na wachezaji wa zamani wa timu hiyo wameonesha kutokufurahishwa na maamuzi ya mwalimu Gareth Southgate baada ya kuwaweka wachezaji hao nje na timu hiyo kushindwa kupata matokeo katika mchezo wa jana dhidi ya Marekani.fodenTimu ya taifa ya Uingereza jana walipata sare na timu ya taifa ya Marekani huku wwakionekana kuzidiwa katika mchezo huo. Jambo hili ndo limefanya watu kuhoji kwanini Foden na Trent wawekwe benchi katika mchezo huo.

Magwiji kama Michael Owen ambaye amewahi kuitumikia timu hiyo ameonesha kusikitishwa na kitendo cha Southgate kuwaweka benchi wachezaji hao na kusema hawjapata matokeo mazuri lakini wachezaji wao wenye vipaji vikubwa wamewekwa nje.fodenPhil Foden na Trent Arnold wamekua wachezaji muhimu zaidi kwenye vilabu vyao lakini inakua tofauti wakienda kwenye timu ya taifa ya Uingereza ambapo wamekua wakipata nafasi finyu ndani ya timu hiyo.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.