Klabu ya PSG imeamua kuingia vitani jumlajumla na klabu ya Manchester kwa mshambuliaji wa klabu ya Atalanta na timu ya taifa ya Denmark Rasmus Hojlund.
PSG wanaripotiwa kua tayari kutoa kiasi cha Euro milioni 60 ili kupata saini ya mchezaji huyo ambaye anawindwa na klabu ya Manchester United kwa karibu zaidi, Huku Mashetani hao wekundu haijafahamika mpaka sasa wamepanga kutoa kiasi gani.Man United inaelezwa wameshamalizana na mshambuliaji Rasmus Hojlund katika masula ya maslahi binafsi, Huku kinachosubiriwa ni kiwango gani cha pesa watatoa kwa mchezaji huyo wakati mabingwa wa Ufaransa wao wameweka kiasi cha Euro milioni 60 tayari mezani.
PSG chini ya mkurugenzi wa michezo Ocampos wanamuona Hojland mwenye miaka 20 kama mshambuliaji ambaye anaweza kufanya vizuri ndani ya timu hiyo, Vilevile anaweza kufiti katika mradi wa kocha mpya wa klabu hiyo Luis Enrique.Manchester United walitaarifiwa wanahofia kua dili lao kwa mshambuliaji Hojlund linaweza kuingiliwa na PSG na ndicho ambacho kinaweza kutokea kwasasa kwani mabingwa hao wa Ufaransa wanaonekana wako makini zaidi kuitaka saini ya mshambuliaji huyo.