Ten Hag: Maguire ni Mchezaji Muhimu Bado

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amemzungumzia alieykua nahodha wa klabu hiyo Harry Maguire kua bado beki huyo ni mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho.

Beki Harry Maguire alivuliwa kitambaa cha unahodha ndani ya kikosi hicho siku kadhaa nyuma kutokana na sababu ambazo aliziongea na kocha Ten Hag, Lakini kocha huyo ameendelea kusisitiza Maguire ni mchezaji muhimu kwenye timu hiyo.Ten HagKocha huyo raia wa kimataifa wa Uholanzi amesema amekua akiongelea suala zima la muendelezo bora wa kiwango kwenye timu, Hivo kama unataka muendelezo bora wa matokeo huwezi kupata ukiwa na wachezaji kumi na moja tu.

Ten Hag anasema kwenye timu yake ana mabeki wanne wa katikati huku Maguire akiwa miongoni mwao na kusema bado anaamini kwenye uwezo wa beki huyo wa kimataifa wa Uingereza kua anaweza kuongeza kitu kwenye timu hiyo.Ten HagTaarifa zinaeleza kua klabu ya Manchester United wanatafuta beki mwingine sokoni, Hivo hii inaonesha kauli za kocha Ten Hag zinaendelea kwani ameshawahi kuwasifu na kusema anawahitaji Ronaldo na De Gea kwa vipindi tofauti na hawakua kwenye mipango yake hii inaweza kutokea kwa Maguire pia.

Acha ujumbe