Martinez pia alisababisha usumbufu kwa mamilioni ya watazamaji baada ya fainali, kwa ishara isiyokuwa nzuri alipotunukiwa tuzo ya golikipa bora wa michuano ya kombe la dunia ‘Golden Glove’.
Shirikisho la Soka la Ufaransa limewasilisha malalamiko rasmi juu ya mlinda mlango wa Argentina Emiliano Martinez kwa kumdhihaki Kylian Mbappe.

Kipa huyo amekuwa akimlenga Mbappe mara kwa mara baada ya timu yake kuishinda Ufaransa kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya 3-3 kwenye fainali ya Kombe la Dunia Jumapili wiki iliyopita.
Martinez kwanza alitoa wito wa “kimya kidogo” kwa Mbappe wakati wa sherehe kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mchezo kukamilika kwenye Uwanja wa Lusail nchini Qatar, kabla ya kufanya vivyo hivyo timu hiyo iliporejea Argentina wakati wa gwaride la ushindi.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 pia alionekana akiwa amebeba mdoli ulivishwa picha yenye sura ya Mbappe wakati wa gwaride huko Buenos Aires, licha ya kusimama kando ya Mfaransa huyo mwenzake huko Paris St-Germain, Lionel Messi.
Rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa Noel Le Graet ameandika barua ya malalamiko akisema kuwa, “Hii inaenda mbali sana, tabia ya Mbappé imekuwa ya kuigwa.”
“Nilimwandikia mwenzangu kutoka Shirikisho la Argentina,” aliiambia Ouest-France. “Ninaona kupindukia kama hii kuwa isiyo ya kawaida, katika muktadha wa mashindano ya michezo, na ninapata shida kuelewa.
Kombe la Dunia la Qatar lilikuwa taji la tatu kwa Argentina, baada ya kushinda mataji mengine mawili mnamo 1978 na 1986 chini ya gwiji wa zamani Diego Maradona.
Bashiri na kitochi au bila bando mechi hii, Bonyeza hapa kutazama ODDS kubwa na bomba kupitia machaguo spesho ya meridianbet ili kuingia mchezoni. Pia ukibashiri na kitochi kwa dau la TZS 1,000/= Unaweza kuibuka mshindi wa MBUZI WA KITOWEO CHA SIKUKUU, kila wiki Ijumaa.

