Kean Ajiondoa Kwenye Kikosi cha Italia

Mshambuliaji wa Fiorentina, Moise Kean amejiondoa kwenye kikosi cha Italia kutokana na maumivu ya mgongo, na Lorenzo Lucca atachukua nafasi yake.

Kean Ajiondoa Kwenye Kikosi cha Italia

FIGC ilisema Jumatatu kwamba mshambuliaji  huyo hatakuwepo kwa mechi za Italia dhidi ya Ubelgiji na Israel mnamo Oktoba.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Juventus alikuwa amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 23 cha Luciano Spalletti kwa ajili ya mechi zijazo za Ligi ya Mataifa ya Roma dhidi ya Ubelgiji na Udine dhidi ya Israel.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Kean Ajiondoa Kwenye Kikosi cha Italia
 

Hata hivyo, Kean anasumbuliwa na maumivu ya kiuno, na kwa sababu hiyo, amerejea katika klabu yake kufanyiwa matibabu.

Spalletti tayari alimuita Lucca kwa ajili ya michezo ya kirafiki nchini Marekani mwezi Machi uliopita, lakini mshambuliaji huyo wa Udinese hakucheza mechi yake ya kwanza kutokana na jeraha dogo. Amefunga mabao matano katika mechi tisa za Udinese katika mashindano yote msimu huu.

Kean ana mabao matano katika mechi 10 alizocheza Fiorentina msimu huu lakini alikosa mkwaju wa penalti dhidi ya Milan jana usiku, huku Spalletti akitazama kwenye viti.

Acha ujumbe