Rais wa PSG, Al-Khelaifi Anaamini Thiago Motta Atafanya Vyema Akiwa Juve

Rais wa PSG, Nasser Al-Khelaifi anaamini Thiago Motta atafanya vyema kama kocha mpya wa Juventus.

Rais wa PSG, Al-Khelaifi Anaamini Thiago Motta Atafanya Vyema Akiwa Juve

Mkuu huyo wa klabu alikuwa nchini Italia kupokea Tuzo ya Uongozi wa Soka katika Tuzo za Globe Soccer.

Akiwa huko, alizungumza na wanahabari ikiwa ni pamoja na Tuttosport kuhusu mabadiliko ya kundi la makocha katika Serie A, ambayo yatamshuhudia Thiago Motta akiondoka Bologna kwenda kuinoa Juve msimu huu wa joto.

“Namtakia kila la kheri, ni mtu wa kipekee ambaye hakika atafanya vyema sana Turin. Alikuwa nasi kwa misimu sita ambayo alishinda mataji mengi na niliweza kuthamini sifa zake za soka na za kibinadamu pia.” Alisema Al-Khelaifi kama alivyonukuliwa na Tuttosport.

Rais wa PSG, Al-Khelaifi Anaamini Thiago Motta Atafanya Vyema Akiwa Juve

Motta wa Italo-Brazil anatimiza umri wa miaka 42 mwezi Agosti na alivaa jezi ya Paris Saint-Germain kama kiungo kutoka Januari 2012 hadi alipostaafu 2018. Hapo ndipo alipoanza mara moja maisha yake ya ukocha akiwa na timu ya vijana ya PSG Under-19 msimu wa 2018-19.

Thiago Motta amefundisha nchini Italia katika kiwango cha juu, akipitia Genoa na Spezia kabla ya kufuzu Bologna kwa ushiriki wao wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa.

Kumekuwa na uvumi kwamba Thiago Motta alikuwa anatazamiwa kuwa na kazi kuu katika klabu ya PSG katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, lakini Al-Khelaifi anasisitiza kwamba hilo halipo kwenye kadi hivi sasa.

Rais wa PSG, Al-Khelaifi Anaamini Thiago Motta Atafanya Vyema Akiwa Juve

“Nina furaha na Luis Enrique, ingawa huwezi kujua maishani …” Alimaliza hivyo Rais huyo.

Acha ujumbe