Klabu ya Simba Sports Club inakaribia kukamilisha dili la kumsajili winga wa AS Vital Club, Elie Mpanzu Kibisawala mwenye umri wa miaka 22. Hii inatokana na klabu hiyo kufanya vibaya kwenye msimu uliomalizika 2023/24 kwa kuambulia nafasi ya 3 inayowapeleka kombe la Shirikisho Afrika. Jisajili na Meridianbet kisha cheza moja ya michezo ya kasino ya mtandaoni, au bashiri michezo mbalimbali kama vile Tenisi, Cricket, Volleyball, Basketball na Handball yote unaipata hapa.
Kwa taarifa zilizopo ni kwamba Elie Mpanzu anatarajia kuwasili Tanzania mara baada ya kumalizika kwa mechi za kufuzu kombe la Dunia za mwezi Juni, ambapo yupo kwenye kikosi cha DR Congo.
Inaelezwa kuwa Makubaliano kila kitu yameshafikiwa ambapo, akija mwezi Juni atasaini mkataba pamoja kuangalia nyumba ya kuishi kabla ya kurejea tena Tanzania kwa ajili ya Pre Season. Meridianbet ni nyumba ya furaha yako, cheza kasino ya mtandaoni na sloti, au bashiri michezo mingi kujizolea mamilioni kila siku.
Elie Mpanzu ni mchezaji anayetumia zaidi mguu wa kushoto kupiga mashuti, lakini pia anatumia na mguu wa kulia, ana sifa ya kushambulia kwa kulifuata boksi la mpinzani huku akiwa na uwezo mkubwa wa kupiga mashuti nje ya eneo la 18.
Pia suala la kuitwa kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo pekee inatosha kuonesha uwezo wake alionao mchezaji huyu, kwani Congo DR imesheheni vipaji vikubwa hivyo kupata nafasi ya kuwa sehemu ya kikosi sio kwa bahati mbaya ni kwa uwezo.