Pigo Jingine kwa SimbaSC ni Hili
Kocha wa magolikipa wa Simba SC Daniel Cadena ameaga rasmi klabuni hapo baada ya kufanya kazi na Simba SC kwa msimu mmoja ambapo alitangazwa kujiunga na timu hiyo mwaka 2023 mwezi wa 7.
Cadena amekuwa katika nyakati nzuri sana akiwanoa walinda milango wa Simba SC na kuinua uwezo na viwango vyao kama Aishi Manula, Ali Salim, Hussein Abel, Ayob Lakred na Ahmed Teru, baada ya mchezo wa mwisho wa Ligi kuu kocha huyo alionekana kwa mara ya pili akigawa vifaa vyake vya michezo vya klabu hiyo kwa mashabiki, ikiwa ni ishara kubwa ya kuwaaga mashabiki.
Kuna Taarifa nyingi zikimtaja kuwa amepokea ofa na vilabu vingi barani Afrika ikiwemo nchini Afrika ya Kusini, huku pia kuna moja ya klabu ya Dar Es Salaam ikiwa inamuwinda mkufunzi huyu raia wa Hispania aliyefanya kazi na vilabu vikubwa Ulaya na Afrika kama, Al Hilal ya Saudia, Azam FC, Simba SC, na RC Recreativo. Mafanikio ya kazi huja kwa bidii, ongeza bidii kwwa unachokifanya itakulipa zaidi haswa ukiweka bidii kubashiri na Meridianbet na kwa kucheza kasino mtandaoni hapa.
Katika ukurasa wake wa Instagram pia aliandika ujumbe huu;
“Leo ni mara ya mwisho ya mafunzo na vijana wangu kutoka SIMBA S.C. katika msimu huu wa 2023/2024. 🥺
“Nimekuwa na bahati ya kufanya kazi na makipa hawa wakubwa na watu wazuri ambao wamejua jinsi ya kuheshimu kazi yangu kila wakati. 👌 Ninajua kwamba wakati mwingine nimekuwa mjinga kwenu, wakati mwingine tumekuwa tukicheka lakini nimefanya kila kitu kwa manufaa ya kila mmoja kwa makipa wangu.”
Kwa ujumbe huu tu ni ishara tosha ya kwamba kocha huyo hatokuwa sehemu ya benchi la ufundi la Simba kwa msimu ujao wa 2024/25, ila inaelezwa kwamba ametoa taarifa kwa uongozi wa Simba hivyo anasubiri majibu kutoka kwenye uongozi wa juu.
Ayob Lakred Kumfuata.
Pia kipa namba moja kwa sasa wa Simba Ayob Lakred inaelezwa kuwa ana ofa ya moja ya klabu kutoka nchini kwao Morocco ikimtaka, lakini nafasi kubwa anaipa Simba SC kwani inaelezwa kuwa yeye binafsi anapenda kuendelea kuishi Tanzania, ila anasubiri Mke wake aje kuangalia mazingira na hali ya hewa ya Tanzania kama ataweza kuishi hapa.
Hata hivyo hatma yake pia itaamuliwa na mustakabali wa kocha wa makipa ambaye amekuwa ni mkufunzi wake wa karibu sana, na lengo la Ayob kubakia Simba alikuwa anataka kucheza Ligi ya Mabingwa kitu ambacho kwa sasa hakiwezekani. Bashiri na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo zaidi 1000.
Simba SC inakumbwa na wimbi kubwa la wachezaji wake kuondoka, huku Mwamba wa Lusaka Chama yeye akiwa kishasinya mkataba mpya utakaombakiza mitaa ya Msimbazi hadi mwaka 2026.