Licha ya mashaka kutoka kwa Roma, Tammy Abraham hataki kuondoka mji mkuu wa Italia msimu huu wa joto kwani anajaribu kujidhihirisha kwenye Serie A kwa mara nyingine tena.
Mshambuliaji huyo Mwingereza mwenye umri wa miaka 26 hakushiriki katika kikosi cha Giallorossi msimu huu baada ya kupata jeraha la maumivu la ligament mwezi Juni mwaka jana, suala ambalo lilimlazimu kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya siku 280. Alicheza kwa dakika 318 tu za mchezo katika mechi 12.
Tammy Abraham aling’ara msimu wake wa kwanza akiwa na Roma, akifunga mabao 17 katika mechi 37 za Serie A, lakini alitatizika kiwango chake katika kampeni yake ya pili, akipachika mabao nane pekee katika mechi 38 za ligi.
Klabu hiyo tayari imeanza kufikiria kumuuza mshambuliaji huyo katika dirisha lijalo la usajili wa majira ya kiangazi. Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.
Ukurasa wa 21 wa Corriere dello Sport leo unaeleza jinsi Tammy Abraham hataki kuondoka Roma msimu huu wa joto, akitaka kujithibitisha kwa Daniele De Rossi katika Serie A msimu ujao.
Kabla ya safari ya Australia, ambapo alifunga katika mechi ya kirafiki dhidi ya Milan, aliwaambia marafiki na familia yake kwamba alitaka kusalia katika mji mkuu wa Italia, akiwa na furaha kikosini licha ya uvumi kuhusu mustakabali wake.