Italia imethibitisha rasmi kumuita Federico Gatti baada ya majeraha waliyoyapata Giorgio Scalvini na Francesco Acerbi.
Mkongwe huyo wa Nerazzurri alijiondoa kwenye kikosi cha Azzurri wiki iliyopita baada ya uamuzi wake wa kufanyiwa upasuaji, na kupunguza chaguzi za Luciano Spalletti nyuma kabla ya Mashindano ya Uropa.
Ndugu mteja kumbuka kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao ambayo inatolewa na Meridianbet. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Mambo yalizidi kuwa mabaya kwa Italia baada ya Scalvini kupata jeraha la anterior cruciate ligament katika mchezo wa mwisho wa msimu wa Atalanta dhidi ya Fiorentina jana, jeraha ambalo litamweka nje kwa muda uliosalia wa kalenda.
Kama ilivyotangazwa rasmi jana, beki wa Juventus Gatti ameitwa na Spalletti kujiunga na kikosi cha Italia huko Coverciano, akiongeza safu ya ulinzi nyuma. Ataungana na wachezaji wenzake wa Italia baadaye leo kuanza maandalizi ya michuano ya Ulaya.
Beki huyo wa kati wa Bianconeri mwenye umri wa miaka 25 amecheza mechi tatu pekee akiwa na Azzurri siku za nyuma, huku mechi yake ya hivi majuzi ikiwa ni ushindi wa 5-2 dhidi ya Macedonia Kaskazini mnamo Novemba.