Mshambuliaji wa AS Roma Tammy Abraham ameongelea kuhusu kurejea kwake kunako klabu yake ya zamani ya Chelsea, ambapo amesema kuwa ana furaha na Roma na anazingatia kazi yake klabuni hapo.

Tammy amesema kuwa Roma ni timu nzuri, kocha wake Mourinho ni mzuri, jiji zuri, mashabiki, na anafuraha hapo Mungu pekee ndiye anayejua yajayo mbeleni kwake labda akiondoka au kusalia.
Kifungu cha Chelsea cha kumnunua Tammy kitakuwa halali kuanzia Julai kwa €80 milioni, ambapo mchezaji huyo aliondoka msimu jana na kujiunga Serie A akionekana hana nafasi kwenye timu hiyo ambayo ilikuwa chini ya Tuchel.
AS Roma mpaka sasa wamecheza michezo nane, wameshinda tano, sare moja na kupoteza mbili wapo nafasi ya sita mpaka sasa.

Mechi ijayo anacheza na Lecce nyumbani kwake ambapo akishinda atapanda hadi nafasi ya nne ya msimamo. Roma kwenye michuano ya Uropa ametoka kupoteza mchezo wake dhidi ya Betis ya Uhispania.
Kifungu cha ununuzi wa Chelsea kitakuwa halali kuanzia Julai kwa €80m.
Picha

